sponsor

sponsor

AddToAny

Slider

Theme images by mariusFM77. Powered by Blogger.

Videos

Music

Story

Business

Jobs

Sports

Comedy

Movie

Health

VIDEO : Mbosso - Picha Yake [Watch/Download]

Hatma ya Nabii Tito aprili 13

KESI  inayomkabili Tito Machibya maarufu Nabii Tito, hatma yake kujulikana Aprili 13 mwaka huu baada ya mahakama ya Wilaya ya Dodoma kupokea taarifa za kitabibu jana asubuhi.

Mahakama ya Wilaya ya Dodoma jana ilipokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya, ilivyokuwa imeviagiza hapo awali na kumtaka afanyiwe vipimo katika Taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma.

Jana Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha alisema mahakamani hapo kuwa alipokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito kutoka Taasisi ya Isanga hivyo ataipitia na kutoa maamuzi siku hiyo ya Aprili 13.

“Nieleze kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa huyu leo asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13 mwaka huu siku ya Ijumaa niweze kuitolea maamuzi,” alisema Karayemaha.

Hata hivyo Nabii Tito jana aliweza kuhudhuria mahakamani akitokea mahabusu ya gereza kuu la Isanga baada ya kutofikishwa mahakamani  hapo  mara mbili mfululizo.

Aidha baada ya kutofikishwa mahakamni hapo hakimu Karayemaha alimwagiza Mkuu wa gereza Isanga kuhakikisha mtuhumiwa huyo anafikishwa mahakamani hapo siku ya jana kusikiliza kesi yake inayomkabili.

Nabii Tito amerudishwa rumande hadi April 13 mwaka huu kesi yake itakapotolewa maamuzi mahakamani hapo.

Nabii Tito anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.

Baada ya kufikishwa mahakamani hapo Nabii Tito alidai kuwa yeye anamatatizo ya akili hivyo mahakama iliamuru kuwa akafanyiwe vipimo vya kitabibu katika taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga Dodoma.

ASLAY - KWA RAHA [Download]





Mbosso - Picha Yake [ Download]




Korede Bello – Work It [Download]

Navy Kenzo – Bhenga [ Download ]

Wema Sepetu: Sioni Wivu Diamond Kumkumbatia Hamisa Mobeto


Wakati habari zilizopo mjini kwa sasa ni tukio la mwanamitindo Hamisa Mobetto na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ’Diamond’ kuteka tukio la utoaji tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF), kwa mrembo Wema Sepetu yeye kaichukulia kawaida.

Diamond na Mobeto katika tuzo hizo zilizofanyika jana ukumbi wa Mlimani City , walikwenda kama wageni waalikwa, walichaguliwa kukabidhi tuzo kwa mshindi wa kipengele cha ‘Best Original Music’ ambayo ilikwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu.

Katika kipengele hicho watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona namna gani Wema ataweza kukabidhiwa tuzo na wawili hao, kwa kuwa filamu yake ya ‘Heaven Sent’ ilikuwa ni mojawapo iliyokuwa ikishindanishwa lakini bahati ndiyo hivyo haikuwa yake.

Akizungumzia namna alivyochukulia  kitendo cha Mobetto na Diamond kufika eneo hilo na kuweza kukabidhi tuzo, Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni kuelezwa kwamba wamerudiana, amesema kitendo hicho kwake amekichukulia kawaida kwa kuwa Mobetto na Diamond ni mtu na mzazi mwenzake.

“Wee ulitaka nichukuliaje labda, Mobetto na Diamond hawa ni wazazi jamani , ulitaka nikasirike au,halafu isitoshe mimi sina uhusiano wa kimapenzi na Diamond  bali ni washkaji tu na siyo kama watu wanavyosema,”amesema Wema.

Kuhusu hatua yake ya kupata tuzo mbili ya msanii bora wa kike na chaguo la watu (People’s Choice Award) kupitia filamu yake ya ‘Heaven Sent’, Wema amesema amefurahi kuona majaji wameweza kuona kipaji alichonacho.

Pia, aliahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake kazi nzuri na kuwaondoa hofu wadau wa filamu waliokuwa wanasema kuwa bongo movie imekufa kuwa siyo kweli bali ilikuwa imelala tu.

Hata hivyo, hakusita kutoa shukurani kwa mashabiki zake ambao amesema ni  kati ya watu ambao waliweza kushiriki kumpigia picha hadi kuhakikisha anapata ushindi huo.