Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana alifanya show kubwa ya uzinduzi wa album yake ya ‘A Boy From Tandale’ nchini Kenya na kukonga nyoyo za mashabiki wake na wadau wa muziki waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Akiwa jukwaani Diamond aliulizwa na MC, kuwa Kenya kuna wasanii maarufu wengi na wengine wakongwe kama Nameless ambaye ana miaka 20 kwenye muziki unawaonaje?
Diamond akajibu “Katika watu ambao kila nikikutana nao kwenye show na kwanza nina bahati ya kukutana naye kwenye show anayokuwepo Nameless anauwa yaani anaperform kichizi kuzidi hata mimi mtoto wa Tandale”.
Onlinejarida's Admin
We are the best publisher in east Africa inoder to keep you up to date
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: