sponsor

sponsor

AddToAny

Slider

Theme images by mariusFM77. Powered by Blogger.

Videos

Music

Story

Business

Jobs

Sports

Comedy

Movie

Health

» » MSUVA AITAKA REKODI YA MBWANA SAMATTA



Simon Msuva (kushoto).
KIUNGO mshambuliaji Mtanzania anayecheza soka la kulipwa Klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, Simon Msuva ametamka kuwa anataka kuifikia rekodi ya mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta.

Kauli hiyo aliitoa baada ya wikiendi iliyopita kui­fanikishia timu yake kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuiondoa Vita SC ya DRC.

Difaa ilifanikiwa kuindoa Vita kwa ushindi wa mabao 3-2 baada ya nyumbani kushinda bao 1-0 lililofun­gwa na Msuva kabla ya kwenda ugenini kupata sare ya mabao 2-2.

Akizungumza na Championi Juma­tano, Msuva alisema rekodi anayoitaka ni kubeba Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mwaka huu kama ilivyokuwa kwa Samatta na Thomas Ulimwengu wal­ivyolichukua wakiwa wanaichezea TP Mazembe ya nchini Congo DRC.

“Ndoto zangu ninaona zinaanza kutimia taratibu ni baada ya kufanikiwa kuiwezesha timu yangu ya Difaa kufuzu hatua ya makundi, niseme kuwa ni jambo jema kwangu.

“Nimeingia kwenye historia moja nzuri kwangu, hivyo sitakiwi kubweteka zaidi ni kuen­delea kuipam­bania timu yangu iweze kuchukua ub­ingwa huu.

“Asante Mungu kwa nafasi ny­ingine sasa ni hatua nzuri hii niliyofikia, kikubwa ninahitaji dua zenu kwani ni wakati mzuri wa mimi kukua na kusogea kisoka,” alisema Msuva.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply