Nondo ameweka wazi hayo baada ya kuachiwa huru na kusema kuwa sasa anaweza kuendelea na masomo yake pamoja na kesi hiyo ambayo itakuwa ikiendelea mkoani Iringa.
"Namshukuru sana wakili Jebra Kombole na wakili wangu mwingine wa Iringa mbali na hapo napenda kuwashukuru wadhamini wangu kwa sababu masharti ya dhamana yalikuwa yanahitaji wadhamini kutoka mkoa wa Iringa kwa hiyo nimepata wadhamini mkoa wa Iringa Mungu awabariki sana, saizi nipo huru naweza kwenda kuendelea na chuo huku nikiendelea na kesi mkoa wa Iringa. Pia nawashukuru Afisa Magereza kwenye eneo ambalo nilikuwa nikiishi katika kusubiria dhamana wamenitunza vizuri kwa upendo na ushirikiano mkubwa hivyo nawashukuru wazazi wangu na Watanzania Mungu awabariki sina zaidi ya zaidi ya hayo" alisema Nondo
Kesi ya Abdul Nondo itatajwa tena tarehe 10 mwezi wa nne mwaka huu mkoani Iringa ambapo wataanza kusikiliza hoja za awali, wakili wa Nondo amewataka watanzani kuwa na subira juu ya jambo hilo kwa kuwa tayari lipo mahakamani hivyo litafahamika.
Onlinejarida's Admin
We are the best publisher in east Africa inoder to keep you up to date
Subscribe to:
Post Comments (Atom)









No comments: