By: MalleBevax
on March 23, 2018
/
Taarifa za kutokea kwa ajali ya lori lililoteketea na moto kwenye Mlima Sekenke mchana huu, mkoani Singida zinaendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, ambao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Mwigulu Nchemba tayari amefika eneo la tukio.
Waziri Mwigulu amefika kuangalia jinsi ajali ya gari hilo la mafuta lilivyoanguka na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu wawili ambao wameungua sana kiasi cha kutotambuliwa hadi sasa huku jitihada zinaendelea kuwatambua.
Kwa mujibu wa shuhuda Edward Lameck, 16, aliyekuwa anapita eneo hilo amesema gari hilo lilifeli break na matairi ya mbele kuanza kuwaka moto hali iliyosababisha gari hilo kutumbukia bondeni na kuwaka moto.
Inaelezwa kuwa imeshindikana watu hao kuokolewa kutokana na kutokana moto mkubwa uliokuwa unawaka. Juhudi zinaendelea kutambua mmiliki wa gari ili kufahamu waliokuwa kwenye gari hilo.
Tag:
Matukio
News
Onlinejarida's Admin
We are the best publisher in east Africa inoder to keep you up to date
No comments: