sponsor

sponsor

AddToAny

Slider

Theme images by mariusFM77. Powered by Blogger.

Videos

Music

Story

Business

Jobs

Sports

Comedy

Movie

Health

» » Ajira 10,000 zatangazwa ujenzi wa bomba la mafuta


Dar es Salaam. Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) imetangaza ajira 10,000 zinazotokana na fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga-Tanzania hadi Hoima nchini Uganda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2018, kaimu mtendaji mkuu wa TaESA, Boniface Chandaruba amesema kati ya kilomita 1,445 za bomba hilo kilomita 1,415 ziko upande wa Tanzania.

"Jumla ya ajira ni 10,000 wakati wa ujenzi na ajira 1,000 wakati wa uendeshaji na katika ajira hizi hakuna gharama yoyote ya kuomba ajira hizi ni bure kabisa na si wote ambao wataomba watapata, itategemea na uhitaji," amesema.

Kaimu mtendaji mkuu huyo ametoa angalizo kuwa, "asitokee mtu yoyote anataka rushwa au aina yoyote ya ushawishi ili kupata hizi ajira atoe taarifa na hatua kali zitachukuliwa."

Amesema licha ya bomba hilo kupita mikoa minane na wilaya 24 ajira zitakuwa kwa Watanzania wote, hivyo wenye sifa za eneo hilo la mafuta na gesi wajitokeze kuomba.

Amesema mwisho wa kutuma maombi ni Machi 30 na mwombaji anaweza kuomba kupitia tovuti yao au kufika ofisi za Kanda zilizopo Arusha, Mwanza au Dodoma.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply