Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amesema kwa sasa hataki tena kusikia mambo ya skendo zaidi ya kufanya kazi tu.
Nay wa Mitego ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Mikono Juu’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kwa mwaka huu anahitaji kutoa ngoma kali pekee na si vinginevyo.
“Huu sio mwaka wa kupigishana na watu kelele ni kazi tu ndio zinakuwa zinaongea, hata kwa wewe mtangazaji ukisikia skendo hata usinipigie simu, so huu ni mwaka wa roho mbaya, panapo majaaliwa next week tutaonyesha huu ni mwaka wa roho mbaya,” amesema Nay.
Hata hivyo licha ya kauli hiyo ya Nay kwa sasa kumekuwepo na stori kuwa Nini na Nay wa Mitego wapo katika mahusiano ya kimapenzi tangu kutoa ngoma yao iitwayo Niwe Dawa ingawa wote wawili hukanusha pindi wanapoulizwa.
No comments: